
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda
RC Makonda amesema kuanzia siku hiyo utaanza msako wa kuwakamata wafanyabiashara wasiokuwa na vitambulisho ndani ya mkoa huo, kwakuwa walipatiwa muda wa kutosha wa kujisajili na kupatiwa vitambulisho hivyo.
Hatua hiyo imekuja baada ya mkuu huyo wa mkoa kubaini uwepo wa wafanyabiashara wanaoendesha shughuli za umachinga bila kuwa na vitambulisho jambo ambalo sio matarajio ya serikali.
Kutokana na hilo RC Makonda amewataka wafanyabiashara wasiokuwa na vitambulisho kufika ofisi za wakuu wa wilaya kuanzia leo Mei 29, 2019, ili waweze kusajiliwa na kupatiwa vitambulisho.