Wednesday , 4th May , 2016

Daktari bingwa wa magonjwa ya Saratani kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dr. Anna Sanyiwa amesema asilimia 80 ya watoto wenye umri kati ya mwaka 1 hadi 5 wanaougua Saratani ya jicho nchini Tanzania hupoteza maisha kila mwaka.

Daktari bingwa wa magonjwa ya Saratani kutoka Hospitali ya taifa Muhimbili Dr. Anna Sanyiwa amesema asilimia 80 ya watoto wenye umri kati ya mwaka 1 hadi 5 wanaougua Saratani ya jicho nchini Tanzania hupoteza maisha kila mwaka kutokana na kuchelewa kupata matibabu ya ugonjwa huo.

Bingwa huyo Dr. Anna Sanyiwa amesema, bado jamii na wauguzi wa afya ngazi ya mkoa na zahanati hawana ufahamu juu ya ugonjwa huo suala ambalo linapeleka waathirika wa ugonjwa huo kuchelewa kupata matibabu na baadae kuwa na upofu au kupoteza maisha.

Saratani ya jicho hutokea kwenye macho yote mawili au kijo moja, ambapo dalili za awali za ugonjwa huo nikuwepo kwa weupe kwenye mboni ya jicho na kwamba ni rahisi kwa familia moja kuwa na watoto wenye ugonjwa huo kwani saratani ya jicho ni miongoni mwa magonjwa yanayo tokana na hitilafu katika vinasaba.

Dr. ameitaka jamii kujenga tabia ya kufanya uchungizi mapema kwani ugonjwa huo unatibika pale wanapo baini mtoto anadalili za macho kuwaka kama ya paka nyakati za usiku, kengeza, weupe kwenye kioo cha jicho, jicho kuivilia damu, kubadilika rangi au kuuma, kuwa kubwa na kuvimba.