Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha,
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha, ameyasema hayo leo katika mahojiano maalum na kuongeza kuwa uzoefu unaonesha hata wakati serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya pembejeo bado zilikuwa hazifiki kwa wakati kwa sababu ya kuwepo kwa mfumo mbaya wa manunuzi ya pembejeo.
Pamoja na kuwepo kwa changamoto za kibajeti kwa msimu huu, wameweka mfumo maalum wa kutumia kampuni ya taifa ya mbolea ili waweze kusambaza kwa wakulima kwa kutumia mfumo huo maalum ambao una ufanisi zaidi ambao utawawezesha wakulima kupata pembejeo kwa wakati.
Amesema kwa msimu huo wakulima wa maeneo mengi nchini wategemee kupata pembejeo bora za kilimo na kufikia uzalishaji wa kimataifa ambao utawawezesha wakulima kiushindani katika uzalishaji na mataifa mengine duniani.




