
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa maendeleo ya jamii Margaret Mussai hii leo jijini Dar es salaam kwenye mkutano wa siku mbili uliowakutanisha wadau mbalimbali wa kutetea haki za watoto ulioandaliwa na shirika la UNESCO ili kujadili haki za watoto na jinsi ya kutekeleza sheria zinazowalinda watoto.
Bi Mussai ameongeza kuwa miongoni mwa haki za watoto zinazojadiliwa ni pamoja na haki ya kulindwa , haki ya kuendelezwa, haki ya kushiriki na haki ya kutobaguliwa lakini kuhusiana na suala la ajira kwa watoto limekuwa kubwa hasa kwa wakati huu ambao maisha yanaonekana kuwa magumu na wazazi au walezi wanaamua kuwatumia watoto wao kama mitaji.
Tatizo la ajira kwa watoto nchini Tanzania bado ni kubwa kwani asilimia 18.7 ya watoto wanatumikishwa na kufanyishwa kazi ngumu hasa sehemu za migodini, mashambani, majumbani na kwenye shughuli za kilimo, hivyo serikali itawachukulia hatua wote watakaoajiri watoto wadogo au kuwatumia kwenye shughuli zao kwa namna yoyote ile.