Wednesday , 11th Mar , 2015

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Christopher Chiza ameitaka Serikali kupunguza Mlolongo wa hatua za kutoa Maamuzi ili kufanikiwa katika kufikia Matokeo Makubwa Sasa katika Sekta za biashara na Uwekezaji.

Waziri chiza ameyasema hayo leo jijin Dar es salaam wakati alipotembelea ofisi za Baraza la Taifa la biashara ili kujionea jinsi baraza hilo linavyoweza kufanya kazi ya kurahisisha uwekezaji.

Waziri Chiza ameongeza kuwa ili Serikali iendane na kasi ya Maamuzi kama katika sekta binafsi lazima mlolongo wa kufanya maamuzi ufupishe hasa kipindi cha biashara ya ushindani na kuwavutia wawekezaji wengi zaidi na kuondoa mazingira magumu ya kufanya biashara hapa nchini.

Kwa Upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la biashara la Taifa Raymond Mbilinyi ameitaka serikali kuiga tamaduni za sekta binafsi ili kufanya maamuzi ya haraka kwa ajili ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Jamii kwa ujumla