Saturday , 3rd Jan , 2015

Mbunge wa Muleba Kusini Prof Anna Tibaijuka amesema kuwa hausiki na aina yoyote ya ufisadi wa fedha zilizokuwa katika akaunti ya Tageta Escrow.

Prof Anna Tibaijuka

Akiongea na wajumbe wa chama hicho wilayani Muleba Mbunge wa jimbo la Muleba kusini Profesa Anna Tibaijuka wakati akiendelea kuwatoa wasiwasi wananchi wake juu ya sakata la Tegeta Escrow amesema kwamba anaendelea kusimamia shughuli za maendeleo katika jimbo lake.

Prof Tibaijuka pia amewataka wananchi kuwa sasa taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu hivyo anahitaji ushirikiano katika kuimarisha chama chake. 
 
Profesa Anna Tibaijuka amesema yeye hakuhusika kabisa katika sakata hilo bali pesa za Escrow alipewa kutoka kwa mfanyabiashara James Lugemala hivyo amewataka watanzania kutosikiliza maneno ya wanasaisa wanaoeneza chuki dhidi yake.

Wakati huo huo, Chama cha mapinduzi kimesema kitawawajibisha watendaji na baadhi ya wafuasi wa chama hicho walioshiriki katika kukihujumu chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mapema akiongea katika mkutano huo, katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Kagera Idd Ally amewataka watanzania kuwa wasikivu ili kulinda amani na utulivu uliopo.

Idd pia amewataka waache kufuata ushabiki wa kisiasa unaonezwa hapa nchini  nakusababisha vurugu za mara kwa mara ambapo amewataka wananchi kutowasikiliza wanasiasa wanaoeneza chuki zinazolenga kuvuruga amani ya nchi.