Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Sina kinyongo na Dkt. Magufuli, atatuvusha-Pinda

Monday , 5th Oct , 2015

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Mhe. Mizengo Pinda amesema yeye hana kinyongo na uteuzi wa Dk. John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Mhe. Mizengo Pinda.

“Tulikuwa wengi kwenyhe kinyang’anyiro cha urais lakini Makamu wa Rais ametolewa, Waziri Mkuu aliyepo ametolewa, Mawaziri Wakuu wastaafu wametolewa, Majaji na mabalozi wametolewa, mawaziri wengine wametolewa; hivi ni kwa nini useme kwamba wewe tu ndiye unayefaa kuteuliwa? Ni kwamba Mungu alikwishamuandaa mmoja wetu,” alisema.

Ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wakazi wa jimbo la Mpanda Vijijini kwenye mikutano minne ya hadhara iliyofanyika katika kata za Kasekese, Kapalamsenga, Karema na Ikola.

“Magufuli ni muadilifu, ni mchapakazi, hana blah blah za kisiasa na hapendi rushwa. Ni mtu anayetaka kuona matokeo na mwenye kujali watu wanyonge. Nimefanya naye kazi kwa muda mrefu, ninamfahamu, ninaomba mumpe kura ya ndiyo ifikapo terehe 25 Oktoba,” alisema Mhe. Pinda wakati akimuombea kura Dk. Magufuli.

Akizungumzia mafanikio ya serikali ya awamu ya nne, Mhe. Pinda alisema Serikali ya CCM imefanya kazi nzuri kwa kufungua barabara za vijijini akitoa mfano wa barabara ya Mpanda hadi Karema ambayo alisema imeboreshwa tofauti na ilivyokuwa miaka 10 iliyopita.

“Wakati huo ukitoka Mpanda kuja Karema ilimchukua mtu hadi siku tatu wakati ni umbali wa km. 150 tu… leo hii mtu anatoka Karema hadi Mpanda na kuunganisha mabasi ya Mwanza siku hiyo hiyo,” alisema.

Alisema katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015, Serikali ya awamu ya tano imepanga kujenga reli mpya ya viwango vya kimataifa (standard gauge) kutoka Kaliua kupitia Mpanda hadi Karema. Alisema anaamini reli hiyo itakuwa ni kiungo cha kuleta maendeleo ya haraka kwenye ukanda huo wa Magharibi.

Alisema Seikali itaendelea kuwaletea maendeleo wanandhi ikiwemo kubotesha huduma za maji, umeme na mawasiliano ya simu.

Aliwataka wakazi wa jimbo hilo watunze shahada za kupigia kura na wasikubali kurubuniwa na mtu yeyote iwe kwa fedha au kitu chochote.

“Usikubali kumpa mtu shahada yaka hata kama ni motto wako. Ninawasihi mjitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura wala msisikilize vitisho vya mtu yeyote kwamba hakutakuwa na amani,” alisema.

Mhe. Pinda alitumia fursa hiyo kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini, Bw. Selemani Moshy Kakoso pamoja na madiwani wa kata zote nne.

Akiwa Karema, Mhe. Pinda alipokea kadi za wanachama waliorejea CCM kutoka vyama vya CHADEMA NA ACT Wazalendo.

HABARI ZAIDI

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala