Friday , 22nd Jul , 2016

Chuo Kikuu cha Sokoine(SUA), kimegundua ugonjwa mpya unaosambazwa na panya ujulikanao kama homa ya Leptospirosis ambao dalili zake zinafafa na malaria,homa ya matumbo na dalili nyingine 40 kwa binadamu.

Panya

Mtafiti kutoa chuo hicho Dkt. Georgies Mgode amesema hayo mbele ya waandishi wa habari na kusema kuwa asilimia 20 ya watu wenye homa ambao hawana Malaria hapa nchini wana ugonjwa huo.

Dkt. Mgode amesema hadi sasa ugonjwa huo haupimiki katika hospitali yoyote hapa nchini na barani Afrika kwa ujumla ambapo nchi za kiafrika zinaonyesha zimeathirika zaidi ambapo watu 95 hadi 100 kati ya laki moja wana ugonjwa huo.

Mtafiti huyo amesema kuwa kitengo cha utafiti na udhibiti wa viumbe hai waharibifu katika chuo hicho kimefaya utafiti wa ugonjwa huo kwa miaka 23 na kugundua kuwa upo kwa wanyama wafugwao kama Ng'ombe, Mbuzi, Kondo,Mbwa na Paka na hata Samaki wa maji baridi.

Aidha amesema kuwa utafiti huo wameufanya katika maeneo ya Morogoro Mjini, Kilosa, Kilombero, Katavi na Kilimanjaro ambapo kwa mkoa wa Morogoro ugonjwa huo kwa binadamu ni kati ya asilimia 10 hadi 15, Moshi ni asilimia 9 na Katavi ni asilimia 30

Amesema kuwa kwa Mkoa wa Morogoro wanyama wenye vimelea hivyo Nguruwe ni asilimia 41,Paka asilimia 14,Panya asilimia 17,kiruka njia asilimia 25,Popo waliokatika makazi ya watu ni asilimi 19 na Samakakii wa maji baridi ni asilimi 54.