
Prof Joyce Ndalichako
Tamko hilo limetolewa leo na Mwenyekiti wa shirikisho hilo Bwana Stanslaus Peter, katika kikao cha pamoja kilichohusisha marais wa vyuo vyote nchini, waliokutana Jijini Dar es Salaam leo, kujadili sintofahamu inayowakumba wanafunzi wanaojiunga mwaka wa kwanza katika vyuo mbalimbali nchini.
Stanslaus amesema kuwa kuna kundi kubwa la wanafunzi ambao wameondolewa kwenye orodha ya wanufaika, na wengine kunyimwa kabisa ama kwa visingizio au bila sababu, jambo linalowafanya waishi katika mazingira magumu na kuhatarisha hatma yao kimasomo.
Amesema wamekubalina kuwa, endapo serikali haitafanyia kazi ombi hilo ndani ya wiki moja, basi shirikisho hilo litachukua hatua ikiwa ni pamojana kuhamasisha wanafunzi wa mwaka wa pili na wa tatu kuungana na wale wa mwaka kwanza katika kudai haki hiyo.
Kwa upande wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kupitia kwa mkurugenzi wake Abdul-Razaq Badru imesema kuwa hadi leo tayari fedha kwa ajili ya wanafunzi wote wenye sifa zimekwisha pelekwa vyuoni, na kwamba bodi hiyo inafanya kazi kwa mujibu wa bajeti iliyopo.