Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini Tanzania - TAKUKURU, Dkt Edward Hosea.
TAKUKURU imependekeza kuifanyia marekebisho sheria ya kupambana na kuzuia Rushwa , ili kosa la rushwa liwe la uhujumu Uchumi na muhusika mwenye mali nyingi anaposhindwa kuthibitisha alivyozipata afikishwe mahakamani na mali zake zitaifishwe.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Edward Hosea, wakati wa majadiliano kwenye semina ya wabunge wa chama cha kupambana na rushwa, amesema kuwa, sheria ya sasa ina mapungufu makubwa hivyo wanaona ni vyema ingefanyiwa marekebisho ili kuipa nguvu ya kuwabana watoa na wapokea Rushwa pamoja na hao wenye utajiri mkubwa.