Monday , 15th Jan , 2018

Tanzania na Msumbiji leo zimekubaliana kuendesha msako wa pamoja dhidi ya makundi ya wahalifu ikiwemo wale wanaojihusisha na vitendo vya ujangili katika maeneo ya mipakani.

Akizungumza mara baada ya kutiliana na saini makubaliano hayo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Msumbiji, Bernadino Rafael, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amesema, uamuzi huo umekuja baada ya kugundua baadhi ya wahalifu wanakimbilia nchi jirani.

Kwa upande wake IGP wa Msumbiji amesema, kuna manufaa makubwa kiulinzi na usalama kushirikiana katika kupambana na wahalifu kwa kuwa watabadilishana ujuzi kulingana na taratibu za nchi zote mbili ulivyo na kuzuia uhalifu.