Akizungumza wakati wa uteketezaji wa bidhaa hizo jijini Dar es salaam jana, Ofisa habari wa TBS, Rhoida Andusamile alizitaja bidhaa hizo kuwa ni dawa za meno, pampas, sabuni za kuogea na wipes.
Akizungumza Jijini Dar es salaam ofisa mdhibiti ubora wa TBS, Salome Emmanuel amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanaingiza bidhaa zenye ubora na wawe walinzi tosha wa kuhakikisha bidhaa hafifu haziingizwi nchini.
Bidhaa hizo ni pamoja na dawa za meno, pampas, sabuni za kuogea na wipes. Miongoni mwa bidhaa hizo zilikuwa ni kwaajili ya kutoa msaada katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara huku nyingine zikiingizwa kwa ajili ya biashara.