Thursday , 12th May , 2016

Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA), imesema inaendelea kusimamia vibali vya uingizaji wa sukari ili kuhakikisha sukari inayoingizwa hapa nchini inakidhi viwango na ni bora kwa matumizi ya binadamu.

Afisa Uhusiano wa (TFDA) nchini, Bi. Gaudensia Semwanza

Hayo yamezungumzwa na Afisa Uhusiano wa (TFDA) nchini, Bi. Gaudensia Semwanza, amesema lengo kuu ni kuwalinda wananchi ambao wanaweza kutumia sukari yoyote kutokana na uhaba wa sukari kwa sasa.

Semwaza amesema kuwa serikali itaendelea kufanya hivyo na endapo watagundua kuna sukari ambayo haikidhi viwango kwa matumizi ya binadamu basi itaondolewa kabisa sokoni.

Afisa uhusiano huyo ametumia fursa hiyo kuwataka waagiziaji wa bidhaa zozote nchini kuangalia vifungashio vya bidhaa hizo kama vimesajiliwa ili kuwapa urahisi mamlaka hiyo kugundua mapema bidhaa ambayo itakua imeingizwa nchini bila vibali maalum.

Kwa upande wa Afisa uendeshaji wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Abel Magese, amezungumzia tatizo la uhaba wa sukari nchini na huku akiishukuru serikali ya awamu ya tano kwa hatua wanayoichukua na kusema wanaimani kwa muda wa miaka mitano viwanda vya sukari vitaweza kutengenweza sukari itakayokidhi mahitaji ya nchi.

Afisa Uhusiano wa TFDA nchini, Bi. Gaudensia Semwanza,