Mtendaji Mkuu wa Chombo cha Utendaji cha Umoja wa Afrika NEPAD, Dkt. Ibrahim Mayaki.
Dkt. Mayaki amesema hayo wakati wa Mkutano Mkuu wa tano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za Umoja wa Afrika zilizopo kwenye mpango huo wa maendeleo barani Afrika.
Mtendaji huyo Mkuu amesema kuwa bara la Afrika kwa sasa lina vijana wengi kuzidi mabara mengine duniani, hivyo kuna nguvu kazi kubwa ambayo isipotafutiwa mpango mahsusi wa ajira umasikini utazidi.
Ameongea kuwa viwanda vingi vya Afrika vikiongezeka ajira kwa vijana zitapatikana, uzalishaji utaongezeka na biashara ndani ya Afrika itashamiri kwa kiasi kikubwa na kukuza nchi moja moja na bara kwa ujumla.
Aidha Dkt, Mayaki amesema changamoto kubwa barani Afrika ni biashara ambapo nchi haziuziani bidhaa zake,miundombinu hafifu na umasikini uliokithiri ambao unaofanya wananchi kushindwa kufanya shughuli za uzalishaji.