Wednesday , 23rd Mar , 2016

Vikundi vya wanawake wajasiriamali nchini Tanzania vimetakiwa kuungana kwa pamoja ili kuweza kusa

Vikundi vya wanawake wajasiriamali nchini Tanzania vimetakiwa kuungana kwa pamoja ili kuweza kusaidiana katika uendelezaji wa biashara ili kuepuka hasara zinazoweza jitokeza.

Akiongea leo jijini Dar es salaam katika mkutano uliowavikutanisha vikundi vidogo vya uwekaji na kukopa vya akina mama katika wilaya ya Kinondoni mjasiriamali wa Kimataifa Bi. Herieth Manase amesema vipo vikundi vingi katika maeneo ya ngazi za wilaya hadi mkoa lakini vyote vinakosa wasimamizi na washauri wazuri wa biashara.

Amesema kwa kutambua hilo yeye pamoja na wajasiriamali wenzake walio katika ngazi ya kimataifa wameanzisha utaratibu wa kutoa elimu ya uwekezaji na ujasiriamali kwa vikundi vidogo vya kuweka na kukopa ili kuweza kuwasaidia katika kuendeleza biashara zao.

Kwa upande wao wakina mama wa kikundi cha uwekaji na ukopaji cha Tandale kwa tumbo wamesema wamekuwa wakichangia na kukopa lakini kutokana na kukosa kwa msingi na elimu ya kutosha kuhusu biashara wamekuwa wakipata hasara na hivyo kushindwa kurudisha mikopo kwa wakati.