
Kamishna wa Elimu, Profesa Eustella
Maamuzi hayo yamefanywa na Kamishna wa Elimu wa wizara hiyo, Profesa Eustella wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam na kusema kuwa amemuagiza Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fedelis Mafumiko kuwavua madaraka wakuu hao kwa kutokana na kukiuka utaratibu wa kuchagua wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza kuwaingiza katika mfumo wa elimu ya watu wazima nchini Tanzania.
Amesema kuwa wakufunzi hao wamekuwa wakishirikiana na halmashauri baada ya kuchagua wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wamefanya vizuri wao huchukua wanafunzi waliofeli na kuwapeleka katika shule za serikali wakidai kuwa wanafunzi wamechaguliwa katika chaguo la pili.
Baada ya kuchaguliwa wanafunzi hao wakifika shule wanadaiwa ada wakati serikali imesema elimu ni bure, hali inayowachanganya wazazi.
Wakati huohuo taasisi ya maendeleo ya elimu Afrika ya Mashariki imekutana kujadili umuhimu wa elimu ya awali kwa watoto katika ujenzi wa taifa na hapa mkurugenzi wa taasisi hiyo Prof. Joe Lugalla anaeleza zaidi.
Adha Prof. Lugalla anatoa angalizo kwa wazazi kujipanga kwa kuwapeleka watoto shule za awali zinazotoa elimu kwa mfumo wa lugha ya kiingereza.