
Kwenye taarifa maalum iliyotolewa kwa vyombo vya habari, imesema kivuko hicho kimeharibika kutokana na kamba na nanga za maboti ya wavuvi kunasa kwenye mitambo ya kuendesa kivuko hiko, na kusababisha huduma kusimama kwa muda.
Kutokana na tatizo hilo Wizara imesema viuko vingine kama Mv. Kazi na Mv. Kigamboni vinaendelea na shughuli za kuvusha watu, huku ikiwataka wananchi wanaofanya shughuli zao za kibinadamu upande wa Kigamboni kutokufanya shughuli hizo karibu na maegesho ya kivuko ili kuzuia tukio kama hilo kujitokeza tena.
Isome taarifa yote hapa
