
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.
Zitto Kabwe ambaye ni moja ya viongozi wa Chama Cha ACT- Wazalendo ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake twitter na kudai kuwa taarifa za kiongozi huyo wa upinzani ni muhimu kwao.
Zitto ameandika, "Mwenyekiti Freeman mbowe leo hajatokea mahakamani, tumesikia ni mgonjwa, poleni sana na tupole wana demokrasia wote nchini, ni muhimu CHADEMA mjulishe umma hali ya Kiongozi wa Upinzani nchini maana tupo nyakati mbaya sana, tusidharau lolote lile".
@ChademaMedia Mwenyekiti @freemanmbowetz leo hajatokea mahakamani. Tumesikia ni mgonjwa. Poleni sana na tupole wana Demokrasia wote nchini. Ni muhimu CHADEMA mjulishe Umma hali ya Kiongozi wa Upinzani nchini maana tupo nyakati mbaya sana Hivi sasa. Tusidharau lolote lile
— Zitto Kabwe Ruyagwa (@zittokabwe) January 17, 2019
Katika kesi ya msingi inayomkabili kiongozi huyo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesogeza mbele hadi Mahakama ya Rufani nchini itakapoamua kesi juu ya kupewa au kutopewa dhamana kwa kiongoz huyo.
Bonyeza Link