
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe akiwa upande wa kushoto, Waziri Mkuu Kassima Majaliwa (kulia).
Zitto ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa twitter mchana wa leo ikiwa umepita muda mchache tokea kumalizika kwa zoezi la uzikaji miili ya wahanga wa ajali ya kivuko cha MV. Nyerere iliyotokea Septemba 20, 2018 katika kisiwa cha Ukara mkoani Mwanza.
"Kwamba mpaka dakika hii hakuna aliye wasilisha barua ya kujiuzulu, Rais hajawajibisha mtu, badala yake Waziri Mkuu anawapongeza kina Mongella na Kamwele kwa kazi kubwa waliofanya. Kazi ya kuacha KUOKOA na kufanya uopoaji, Waziri Mkuu tunakuheshimu sana lakini kwenye hili si sawa", ameandika Zitto.
Kwamba mpaka dakika hii hakuna aliye wasilisha barua ya kujiuzulu, Rais hajawajibisha mtu, badala yake Waziri Mkuu anawapongeza kina Mongella na Kamwele kwa kazi kubwa waliofanya. Kazi ya kuacha KUOKOA na kufanya UOPOAJI? Waziri Mkuu tunakuheshimu sana lakini kwenye hili SI SAWA
— Zitto Kabwe Ruyagwa (@zittokabwe) September 23, 2018
Ajali ya kivuko cha MV. Nyerere kilichozama Septemba 20, 2018 kimesababisha takribani watu 224 kufariki ambao kwa sasa wamezikwa katika makaburi ya pamoja yaliyopo viwanja vya shule ya sekondari ya Bwisya mita 250 kutoka gati la Bwisya.
Hadi sasa serikali imeshaanza kuchukua hatua madhubuti ya kukitoa kivuko hicho majini kwa kutumia burudoza lililowasili katika kisiwa cha Ukara, wilayani Ukerewe na limeanza zoezi la kuvuta kivuko hicho katika Ziwa Victoria, na kukipeleka nchi kavu ambapo zoezi hilo linatarajiwa kukamilika kwa muda wa wiki moja tokea sasa.