Monday , 30th Mar , 2015

Maziko ya aliyekuwa Muasisi wa Kundi la Tip Top Connection, Marehemu Abdu Bonge yanatarajia kufanyika siku ya kesho Makuyuni Mkoani Morogoro, baada ya zoezi la uchunguzi wa mwili wa marehemu na shughuli za uagaji kukamilika hapa jijini Dar.

mwili wa muasisi wa kundi la Tip Top Connection Abdu Bonge

Shughuli hiyo imefanyika nyumbani kwa marehemu Magomeni Kagera na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa waombolezaji ambao wameguswa kwa namna moja au nyingine kutokana na kifo hicho cha Marehemu Abdu Bonge.

Marehemu Abdu Bonge amepoteza maisha usiku wa juzi baada ya kusukumwa na kuanguka alipokuwa akiamua ugomvi wa majirani zake, na eNewz tunaiombea roho ya marehemu mapumziko mema mahala pema peponi, Aamin.