
Gigy Money na Wizkid
Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live 'FNL' kinachorushwa na East Africa Radio na East Africa Television, Gigy Money amesema ana imani ndoto yake hiyo ipo siku ataitimiza kama alivyoitimiza kwa Tekno, na lazima atawathibitishia umma kuwa ameitimiza ili asichekwe.
"Namkubali kinoma yani, ntabeba tshirt alafu ntaunganiha mapicha, ntawaambia jamani, mnakumbuka hii alishutia video fulani, hii hapa, mimi niko 'serious' na mpambano wangu nimekamilisha, mimi huwaga napenda tu kuwahakikishia lakini wao wanafikiriaga vingine, unajua ndoto siyo wote wanatimiza", alisema Gigy Money.
Gigy Money alisema hata kwa msanii Tekno alikuwa na ndoto kama hiyo na alihakikisha ameitimiza, na kuweka ushahidi mezani.
Msikilize hapa akipiga stori na mtangazaji Sam Missago wa EATV akimkamia kumpata Wizkid.