Thursday , 14th Aug , 2014

Mrembo aliyewahi kushikilia taji la Miss Sinza mwaka 2011, Husna Maulid amesema kuwa, amejipanga kusaka vijana wenye vipaji mbalimbali katika jamii ili kuwasaidia kuondokana na tatizo la kutokuwa na ajira.

Miss Sinza 2001 Husna Maulid

Husna ambaye pia ni Video Queen mahiri, amesema kuwa, mpango huu upo katika hatua za awali kabisa na hivi karibuni atautangaza kiundani, na hii yote ikiwa ni lengo la kuwakwamua vijana na kuwapa nafasi ya kutumia uwezo walio nao kuendesha maisha.