Saturday , 6th Sep , 2014

Siku ya leo onesho kubwa la Kilimanjaro Music Tour ndiyo gumzo la Jiji la Dar ambapo kuanzia sasa tunakutana pale Leaders Club hapo wapenda Burudani wote kusherekea muziki wa kikwetu kwetu.

Jambo Squad jukwaani

Wiki hii nzima timu ya eNewz ikiambatana na timu ya East Africa Radio imekuwa mtaani kuongea na kuwazawadia mashabiki ambao wameweza kujibu maswali kuhusiana na tukio hili kubwa.

Zoezi hili limeendeshwa pia kwa njia ya mitandao ya kijamii, www.facebook.com/eatv.tv na twitter @eastafricatv ambapo baadhi ya washindi wa huko ni Netta Ngeleshi na Partson Mutayoba ambao nao walijipatia zawadi zao tayari kwa kushiriki show leo.

Kumbuka, milango ipo wazi kuanzia sasa, ni pale Leaders Club, tunasogea pale kushuhudia, wasanii sio chini ya 14 wakitumbuiza juu ya Jukwaa, akiwepo Christian Bella, Mashujaa Band, Khadija Kopa, Jambo Squad, Ben Pol, Proffesa Jay, Rich Mavoco, Vanessa Mdee , AY, FA Weusi pamoja na Jose Mara na Bendi yake. Na kiingilio katika onesho hili ni shilingi 3,000 tu, na unapatiwa kinywaji chako bure mlangoni halafu Tunazungusha Kikwetukwetu.