Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Lulu afichua mazito siku ya kifo cha Kanumba

Monday , 23rd Oct , 2017

Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili muigizaji wa filamu Tanzania, Elizabeth Michael (Lulu), imeendelea leo ambapo upande wa mshtakiwa umeanza kutoa utetezi wake.

Akisimulia jinsi ilivyokuwa siku ya tukio, Lulu amesema marehemu alikuwa akimpiga na panga baada ya kutokea ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi, alipomuona akiongea na simu.

"Nilikuwa nataka kutoka ila marehemu 'Kanumba' alinikataza, alikuwa hataki nitoke, nilipomwambia natoka na marafiki zangu alinikimbiza na taulo na mimi nilikuwa naogopa kupigwa, mara nyingi alikuwa ananipiga kila akilewa na sio kwa akili zake, alipoona simu yangu inaita akahisi ni simu ya mwanaume akasema kwanini naongea na simu ya mwanaume mbele yake? Marehemu akaingia uvunguni akatoa panga akasema leo nakuua huku akinipiga na panga kwenye mapaja", ameelezea Lulu.

Lulu ameendelea kusimulia...."Marehemu alianguka mwenyewe na kujigonga kwa nguvu na kuinuka sehemu nyingine alikuwa kama anatapatapa, nilimwambia Seth kuwa Kanumba amedondoka na akajaribu kumuamsha hakuamka akasema anaenda kumuita daktari, alivyosema anaenda kumuita daktari na mimi nikaondoka nikiogopa anaweza akaamka akaanza kunipiga, niliondoka nikawasha gari kuelekea Coco Beach kutuliza akili".

Muigizaji huyo ameendelea kusimulia kwamba ..."Nilivyofika Coco beach meseji zilianza kusambaa kuniuliza kuwa nasikia Kanumba amefariki, nikampigia 'Kidume'  ambaye ni rafiki yake Kanumba kumuuliza Kanumba yupo hospitali gani niende kumuona, akaniambia wewe usije hospitali, niambie uko wapi, tukakubaliana tuonane Bamaga, tulivyokutana Bamaga alikuwa kama anataka kuongea na mimi ghafla wakaja askari kunikamata".

Pamoja na hayo muigizaji huyo ameithibitishia mahakama kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu (Steven Kanumba) kwa muda wa miezi minne kabla ya kukutwa na mauti.

Mahakama Kuu imehairisha kesi hiyo mpaka siku ya kesho Oktoba 24, ambapo itasikilizwa tena.

 

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa