Thursday , 16th May , 2019

Msanii wa Kisingeli Manfongo,  amevunja ukimya na kuzungumza na eNewz na kusema kuwa yeye hajahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.

Msanii Man Fongo

Hivi karibuni mitandaoni ilisambaa taarifa kuwa msanii huyo aliyewahi kufanya vizuri na ngoma yake ya Hainaga Ushemeji, amefungwa kwa kosa la kumpa ujauzito mwanafunzi wa shule.

Fongo mwenyewe ameeleza kushangazwa na habari hizo huku akitangaza kumtafuta mtu aliyeanzisha habari hizo za kumchafua.

Zaidi mtazame hapa.