Wednesday , 5th Jul , 2017

Msanii Mkongwe Captain Tundaman amedai yeye anawaimbia watu waliokata tamaa na maisha ndiyo maana kila siku anasikika kama mtu anayelalamika kwenye nyimbo zake hata pale anapoimba kuhusu mapenzi.

Captain Tundaman

Tundaman amesema hayo leo kwenye 5SELEKT ya EATV na kusema kwamba wateja wa nyimbo anazoimba ni watu wenye maisha ya kawaida sana na wanaohitaji kuwakilishwa.

"Siku zote mtu ambaye amekata tamaa au mwenye maisha magumu huwa analalamika sana. Haijalishi kuwa ni kwenye mapenzi au maisha ya kawaida, watu wa Masaki hawawezi kulalamika kuhusu njaa lakini wanaweza wakawa wamekata tamaa kwenye mahusiano hivyo mimi nawawakilisha wenye matatizo" , Tundaman alisema

Baada ya kimya kirefu Tundaman amerudi na ngoma inayokwenda kwa jina 'Shauri Yako' aliyomshirikisha msanii mchanga.