.jpg?itok=n6HSv33q×tamp=1490887612)
Maua
Mrembo huyo amesema kazi yake ya muziki imekuwa ikimfanya aweze kujitegemea katika mambo mengi anayotaka kuyafanya akiachana na elimu aliyoipata akiwa darasani.’
“Muziki ni mzuri na ninaupenda sana ndiyo maana unaona kila nikiimba ninaimba kwa hisia sana. Hii ni kutokana na mimi mwenyewe kuipenda kazi yangu vilevile, muziki unalipa tena sana, mimi umeweza kuniletea mafanikio mengi moja wapo likiwa ni kuagiza gari aina ya 'IST New Model' ambalo nategemea hivi karibuni litaingia nchini kutoka nilipoagiza". Alisema Maua
Aidha Maua amesema ucheshi wake, upole na heshima umemfanya ajione tofauti na wasanii wengine wanaoimba ambao baadhi yao huwa hawaheshimu kazi yao wanayoifanya.
Kwa upande mwingine msanii huyo ameingia katika orodha ya wasanii wanaotarajia kuachia albam yake licha ya wasanii wengi kuhofia kuwekeza kwenye albam.