Wednesday , 17th Jun , 2015

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Maurice Kirya amejikita katika kunyanyua vipaji vya uigizaji, akitoa nafasi kwa mashabiki zake wenye uwezo katika fani hiyo kuwasiliana naye ili kupata shavu la kushiriki katika projekti yake ya maigizo.

Maurice Kirya

Katika hatua ya awali kabisa ya mpango huo, Kirya ametangaza uhitaji wa mwanamke mwenye umri kati ya miaka 23 na 30, na mwanaume mwenye umri kati ya miaka 40, na mwingine mwenye umri kati ya miaka 30 kwa ajili ya kazi hiyo.

Mkakati huu unaoendeshwa na Kirya kwa njia ya mtandao, unatarajiwa kuwa ni fursa nyingine kubwa ya kuvimulika vipaji kutoka mitaani, na kuvipatia nafasi ya kutumia kwa manufaa uwezo wao wa kuigiza.