Thursday , 11th Sep , 2014

Aslay kutoka kundi la Mkubwa na Wanawe la Yamoto Band, amesema kuwa albam ambayo inapikwa sasa kutoka katika kundi hili itahusisha wasanii kutoka nje ya mipaka ya Tanzania huku akijiandaa kufanya kolabo na kundi la Sauti Sol la nchini Kenya.

msanii wa muziki wa bongofleva Aslay

Aslay ameiambia eNewz kuwa, albam hii ambayo tarehe ya kutoka kwake itatangazwa rasmi na Menejimenti, Mkubwa na Wanawe vilevile kukiwa na kazi ambazo wamefanya na vichwa vikali kutoka hapa hapa Bongo.

Aslay pia akawatonya mashabiki wale wanaosikilizia kazi zao wakiwa solo kuwa kwa sasa nguvu zao nyingi wamewekeza katika kuisimamisha Bendi Vizuri kabla ya kuachia kazi binafsi.