Monday , 31st Oct , 2016

Rapa Mr Blue ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake 'Mboga' saba aliomshirikisha Alikba amefunguka na kusema muziki wa bongo sasa unalipa ndiyo maana ameweza kuwa na nyumba zaidi ya mbili na sasa anajenga nyumba nyingine Tabata Kinyerezi.

Kutoka kushoto ni Abby Skillz, Mr. Blue na Sam Misago katika FNL

Akiongea kupitia kipindi cha Friday Night Live (FNL) Mr Blue alisema kuwa kupitia kazi yake ya muziki ndiyo imeweza kumpa mafanikio hayo na kuweza kumiliki nyumba zaidi ya mbili na sasa anajenga nyumba nyingine Kinyerezi mbali na mali nyingine alizonazo zinazotokana na muziki huo huo.

"Unajua mimi ni most expensive MC ambaye nashindana na hawa wasanii wa kuimba, muziki saizi unalipa sana ndiyo maana unaona watu wanajenga na kuwa na maendeleo mimi saizi hapa nina nyumba zaidi ya mbili ambazo zimetokana na kazi yangu hii ya muziki na bado najenga nyumba nyingine Tabata Kinyerezi ambayo ndiyo nataka kuhamia huko sasa" alisema Mr Blue