Monday , 14th Aug , 2017

Msanii Nay wa Mitego ambaye anajulikana kwa kuwa na maneno ya uchokozi kwa wasanii wenzake, leo kakutana na aliyemzidi na kumfanya awe mpole kama ananyolewa.

Ney na Dudu Baya

Ikumbukwe wiki iliyopita msanii Dudu Baya ambaye wasanii wenzake wengi wanamuogopa kwa kuwa ni mtu wa ngumi mkononi, alimfananisha Nay wa Mitego na kina Gigy Money na Amber Lulu, na kumuonya asithubutu kujilinganisha na wasanii kama Godzilla kwani hana ubavu wa kushindana nao kwenye muziki.

Mtandao wa EATV ulifanya jitihada za kumtafuta Nay wa Mitego ili aweze kujibu tuhuma hizo za kufananishwa na wasanii kama Gigy Money ambao ni wasanii wa kike, na kuonekana kuruka viunzi kumjibu Dudu Baya, huku akisema mwambieni anakubali kwa alichokisema kwamba yeye ni sawa na Amber Lulu.

Msikilize hapa Nay akikiri kufananishwa na Amber Lulu.