Tuesday , 10th May , 2016

Msanii anayechipukia kwa kasi katika bongo fleva Kayumba Juma hawezi kusahau tukio la kufukuzwa kwenye nyumba ya ndugu yao akiwa na baba yake mzazi

Msanii wa Bongo fleva Kayumba Juma

Akizungumza na Enewz Kayumba alisema kuwa tukio hilo ndiyo chanzo pekee kilichomfanya ajitume zaidi ili aweze kufanikiwa.

“Kile kitu kiliniuma sana na siwezi kusahau katika maisha yangu kwasababu tulifukuzwa kama mbwa na tulikuwa hatujui tutaenda kufikia wapi”, alisema Kayumba.