
Muigizaji, Elizabeth Michael
Uamuzi wa Lulu umekuja leo ambapo katika ukurasa wake wa Instagram amebainisha akisema kwamba ataitumia siku ya wapendanao, Februari 14 kuuza nguo zake.
"Wakati wengine tumepata fursa ya kuwa na furaha kwa vile tulivyonavyo kuna baadhi ya wenzetu wamekosa nafasi hiyo na huu ni mpango wa mungu," Lulu.
Lulu ameongeza kwamba, "Kuelekea siku ya wapendanao Februari 14, nimeamua kuuza sehemu ya nguo zangu ambazo yawezekana umeshawahi kuziona au haujaziona na pesa yote itakayopatikana kupitia mauzo haya itaenda kusaidia vitu/watu wenye uhitaji katika jamii. 'Please Join me to save my Valentine".
Hivi karibuni Lulu kupitia mtandao wake wa Snapchat aliweka wazi kwamba anahitaji kugawa nguo zake kwa mashabiki wake jambo ambalo lilivutia wafuasi wake kiasi cha kufanya watu wengine kumkumbusha.