
Star wa muziki wa Rap Bongo Roma Mkatoliki
Akizungumza na eNewz Roma alisema kuwa hayo ndiyo maisha aliyoyachagua na ni mwanaharakati anaetetea haki na amani katika taifa lake, maendeleo bora na hicho ndicho kitu kikubwa anachojaribu kukipigania.
“Natamani nipate utawala au uongozi ambao utamfanya Roma asiimbe hip hop na ukiona kila siku Roma anatoa mawe basi ujue bado hatujapata uongozi huo ama utawala huo," alisema Roma na kuongeza, "Kwa hiyo inabidi niendelee kushindilia ili taifa langu siku moja lione kwamba Roma alikuwa ni mmoja kati ya wapigania haki”.