
Shilole
Akiongea kupitia eNEWZ Shilole amesema anachukizwa sana na vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikikazana kuwapatia umaarufu watu ambao hawana sifa za kuwa wasanii na kujikuta mwisho wa siku wanaharibu kabisa sifa ya sanaa na kuharibu 'brand' za wasanii wengine waliojituma zaidi kwenye sanaa zao ili kujitengenezea umaarufu.
"Kwa kweli mimi naumia sana ninapoona kuna watu sijui ma 'video vixen' ambao wameonekana kwenye video moja halafu wanaitwa wasanii nguli ambao wakati ukiangalia hakuna kazi yoyote ya kueleweka ambayo wameifanya kwa jamii, kwa kweli mimi naomba vyombo vya habari viangalie watu wa kuwapa umaarufu ili kulinda 'brand' zetu"aliongea Shilole.
Pia Shilole amefunguka kuhusu juhudi zake za kutaka kupungua na kubadilisha muonekano wake na kudai alishafanya mazoezi na kuacha baada ya ratiba zingine kuingilia na pia alikiri kuwa mwili wake ulivyo sasa haumpi tatizo kwani ni mwepesi na hapati shida katika kazi zake lakini anatarajia kurudi 'gym' ili kutengeneza mwili wake vizuri.