Tuesday , 16th Jan , 2018

Msanii wa Hip hop 'Ben Gang' amemjia juu msanii anayefanya vizuri kwenye Singeli, Man Fongo baada ya kuchukua melody pamoja na mashairi ya wimbo wake kisha kuuachia kama ngoma yake. 

Msanii Ben Gang amedai kuwa  Man Fongo kwa mara ya kwanza aliyasikia mashairi yake walipokuwa kwenye 'show' India na kuongeza kuwa itakuwa aliyakubali na kuamua kuyaweka kwenye mtindo wa Singeli.

Akizungumza na story Tatu ya Planet Bongo msanii huyo wa Hip hop amesema kwamba anachotaka ni msanii huyo kuomba radhi kwenye 'media' kama jinsi ambavyo amekuwa akiutangaza wimbo kama wake ikiwa ni pamoja na kuufanyia video ilihali anafahamu kwamba siyo wake.

"Ninachokumbuka tukiwa India tulifanya Show kubwa na hawa majamaa. Nadhani alipenda ngoma yangu....Sasa leo nimekaa ofisini kuna watu wananipigia simu na wengine kunionyesha kuwa jamaa kafanya remix ya wimbo. Hajaongea na mimi walala nini. Sasa mimi ninachotaka ni azunguke kwenye media akaombe radhi kwa tukio hili alilolifanya" Ben Gang.

Ameongeza kwamba kinachomshangaza ni Manfongo kuchukua mashairi ya hip hop mpaka kwenye Singeli na kudai kuwa amekasirishwa na kitendo hicho la sihivyo 'Atamchimba'.

Juhudi za kumpata Man Fongo ziligonga mwamba baada ya kutopatikana kwenye simu yake ya mkononi ikiwa ni pamoja na kuingia mitini alipotakiwa kufika kwenye kipindi cha Planet Bongo.