
Jay Moe amefafanua hayo baada ya kuenea tetesi zilizokuwa zikiwaaminisha watu kuwa huenda akasainiwa na Mr T-Touch ili aendelee kutoa nyimbo chini ya uongozi wa 'Producer' huyo.
"Mimi ni C.E.O wa so Famous entertainment kwa hiyo siwezi kusainiwa na mtu mwingine wakati mimi mwenyewe nataka kusaini watu, mimi sipo kwa T-Touch wala sipo tayari kusainiwa na 'record label' yoyote kwa sababu nina label nataka niikuze nisaidie wengine ambao wapo nyuma yangu, wanataka waone mafanikio yangu ili na wao yawanufaishe" - alisema Jay Moe
Mtazame hapa chini akiendelea kufunguka mengine zaidi...