
Ruby amefunguka hayo wakati akijibu maswali ya kuhusu kuweka picha mtandaoni zilizosababisha utata wa um,bo lake tofauti na alivyozoeleka.
Ruby amesema kwamba kupitia simu msanii anaweza kujiremba kwa jinsi ambavyo ataweza kusababisha mashabiki zake waendelee kumfuatilia na hata kumjadili.
"Zile picha zenye kunionyesha umbo kwanza alinitengenezea shabiki yangu akanitumia kisha mimi nikaona niiweke mtandaoni kama somo kwa wasanii wenzangu. Unaweza kufanya kitu kama ile na ukapata attention uliyokuwa unaitaka. Badala ya kupiga picha za utupu na kwa sasa serikali iko macho siyo vizuri. Napenda tuwe wabunifu" amesema Rubby..