Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Kimya cha CHADEMA kina kishindo – Dkt. Mashinji

Wednesday , 26th Oct , 2016

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Vincent Mashinji amewatoa hofu wapenzi na wanachama wa chama hicho kwa kuonekana kuwa kimya, ambapo amesema kwamba chama hicho kinajipanga.

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Vincent Mashinji

Amesema amesema kwa sasa chama hicho kinaendelea na kazi zake za kujiimarisha kila kona nchini na kuwatetea wananchi katika masuala mbalimbali ya maendeleo.

Dkt. Mashinji ameyasema hayo katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa na EATV kupitia ukurasa wake wa Faceebook, wakati akijibu maswali ya wananchi.

Amesema chama hicho kimeanza mikakati ya kushinda uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020 na kuwataka wananchi kuendelea kukiunga mkono chama hicho na kubainisha kuwa kwa sasa wameanza kuwekeza nguvu vijijini ili kuhakikisha chama kinasikika kuanzia ngazi ya msingi wa familia.

“Wananchi wanauliza kwamba tumepoa, siyo kweli ukimya wetu una kishindo , tunajipanga kufanya mambo mbalimbali na mikakati hiyo siyo vyema kuiweka hapa, lakini hivi karibuni wananchi wataona uwakilishi  wetu kwao, CHADEMA ipo imara” Amesema Dkt. Mashinji.

“Tunajipanga kukamata dola mwaka 2020 na tunawaomba watanzania kuendelea kutuunga mkono kwani nia yetu ya kuiongoza taifa hili kuwa na uchumi imara na kuhakikisha maisha ya wananchi yanaimarika upo palepale” Amesema Mashinji.

Aidha Mashinji amesema Baraza la Vijana la CHADEMA ,BAVICHA na Baraza la Wanawake BAWACHA wote wamejipanga vizuri katika kuhakikisha kwamba chama kinaenea kwa wananchi kuanzia ngazi ya chini.

Aidha Mashinji amesema CHADEMA huwa haisusii vikao halali ambavyo huwakutanisha na chama tawala CCM ila pale ambapo huona vikao husika havina nia ya kutaka kutenda haki ndipo hujitoa katika vikao hivyo na kuwataka wananchama kuendelea kuwa na imani na chama hicho.

HABARI ZAIDI

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala