Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Nilikaribishwa Freemason nikakataa - Rammy Galis

Wednesday , 19th Oct , 2016

Star wa Bongo Movie Rammy Galis amefunguka na kukiri kuwa kuna watu hususani wasanii wanaojihusisha na kundi la Freemason na kwamba yeye mwenyewe aliwahi kualikwa kwa njia ya simu yake ya mkononi ajiunge na kundi hilo lakini alikataa.

Msanii wa Filamu nchini Rammy Galis

Akizungumza katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa LIVE kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV, Galis amesema yeye hajajiunga na Freemason na wala hatafanya hivyo lakini alishawahi kutumiwa ujumbe wa kujiunga.

Galis alikuwa akijibu swali kutoka kwa mmoja ya mashabiki wake aliyetaka kujua iwapo Diamond pia yupo katika kundi la Freemason au illuminati kama ilivyokuwa ikidaiwa kwa marehemu Steven Kanumba, ambapo alisema kuwa yeye hawezi kufahamu, na kukiri kuwa suala hilo kwa wasanii lipo na ni la kawaida.

“Kwa kuwa nimeulizwa, ngoja nijibu, ukweli kuna siku nilipata meseji kama ilivyo kwa ujumbe wa tigo pesa au M-Pesa, iliyokuwa na kichwa kilichosomeka Freemason, ujumbe huo ulinitaka nijiunge na Freemason, kama niko tayari kujiunga na biashara hiyo nijibu ujumbe huo na kama sitaki nifute ujumbe huo, nilipojaribu kufuatilia zile namba zikaonesha kwamba hazitambuliki (Unknown number), basi nikaufuta na wala sijafuatilia tena, kwahiyo kuhusu Diamond, mimi sijui" Amesema Galls

Aidha msanii huyo amesema anatarajia kuachia filamu kali mwezi Desemba mwaka huu na kuwataka wananchi kumuunga mkono kwani itakuwa na ubora wa hali ya juu na kwamba ameitengenezea nje ya nchi na wasanii wakubwa wa Nigeria.

Pamoja na hayo Rammy Galis amewataka wasanii wa Bongo Movie kukaza katika soko la sasa na kuto kata tamaa kwani mafanikio hayaji bure bila kuweka juhudi za makusudi .

HABARI ZAIDI

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala