Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

 Miji iliyotembelewa zaidi duniani mwaka 2018

Tuesday , 25th Sep , 2018

Binadamu huitaji mazingira mapya katika kupumzisha akili yake baada ya kufanya shughuli mbalimbali kwa muda mrefu, wengi hutembelea miji mbalimbali aidha kwa shughuli za kiutalii ama katika mihangaiko ya kazi.

Kampuni ya Mastercard imetoa listi ya miji mbalimbali ambayo imeongoza kwa kutembelewa zaidi mpaka sasa ndani ya mwaka 2018, ambapo mji wa Bangkok kutoka nchini Thailand umeendelea kubakia katika nafasi za juu kutoka mwaka uliopita, ikiwa na ukuwaji wa uchumi kwa asilimia 9.7.

Hii hapa ni listi ya miji 10 ambayo inaongoza kwa kutembelewa zaidi duniani mpaka sasa ndani ya mwaka 2018.

Bangkok, Thailand

Mji huo ambao umekuwa  maarufu kwa miaka mingi kutokana na vyakula vyenye viungo mbalimbali na mahekalu ya jamii ya Buddhi, umetembelewa na watu zaidi ya 21.9 millioni kutoka nje ya nchi ndani ya mwaka huu. Lakini hivi sasa inatajwa kuwa watu wanatembelea zaidi kwaajili ya manunuzi ya vitu mbalimbali yakiwemo ya vitu vya thamani. Duka maarufu la bidhaa nchini humo linalojulikana kama 'Siam Paragon shopping mall' , ni eneo ambalo liliwahi kuwa la pili kwa umaarufu katika mtandao wa Istagram kwa takwimu ya mwaka 2013.

London, Uingereza

Mji huo umetembelewa na watu zaidi ya 20.4 millioni mpaka sasa katika mwaka huu huku baadhi ya vitu vinavyowavutia watu wengi katika mji huo ni pamoja na matukio ya kimichezo ikiwemo ligi ya kuu ya nchi hiyo (EPL) ambayo ni ligi maarufu duniani, daraja lijuliakanalo kama 'Tower Bridge' ambalo lina historia tangu karne ya 19, 'London Eye' na kwaajili ya manunuzi mbalimbali.

Paris, Ufaransa

Mji huo umeshatembelewa na watu 17.9 millioni mpaka sasa katika mwaka 2018 ambapo kivutio kikubwa ni mnara wa Eiffel ambao unashikilia historia ya kuwa moja kati ya minara mrefu zaidi duniani. Vivutio vingine vinavyowavutia watu wanaotembele mji huo ni katika matukio ya kimichezo, kama mashindano ya Tenisi ya French Open na michezo ya soka ya ligi ya Ufaransa, Ligue 1.

Dubai, UAE

Mji huo umetembelewa na watu takribani 16.6 millioni mpaka sasa ndani ya mwaka 2018 ambapo wengi kati hao wametembelea kwaajili ya shughuli za utalii ikiwemo kutazama madhari ya mji huo ambao umejengwa kwa ustadi wa hali ya juu pamoja na kufanya manunuzi mbalimbali ya vitu vya thamani hasa vyevye tamaduni za kiarabu ambapo wastani wa matumizi ya wageni hao kwa mwaka huu ni dola 537 kwa siku ambayo ni sawa na 1.2 millioni za kitanzania.

Singapore

Visiwa hivyo vimevutia watu takribani 14.4 millioni mpaka sasa. Watu wengi wanavutiwa na utalii katika visiwa hivyo ambapo maeneo yanayovutia watu wengi ni kama Singapore zoo, makumbusho ya visiwa hivyo yakiwemo mahekalu ya kibuddha, kilele cha mlima Faber ambacho kinaonesha kwa ufasaha maemeo yote ya mji, eneo maarufu la kuogelea la 'Jurong East' na maeneo mengine mengi.

Miji mingine iliyotembelewa na watu wengi mpaka sasa duniani ni pamoja na New York(Marekani) ambao umetembelewa na watu 13.6 millioni, Kuala Lumpur(Malaysia) ukiwa na idadi ya watu 13.5 millioni waliotembelea, Istanbul(Uturuki) ukitembelewa na watu 12.8 millioni, Tokyo(Japan) wenye watu 12.2 millioni waliotembelea pamoja na Antalya(Uturuki) uliotembelewa na watu 11.2 millioni mpaka sasa.

HABARI ZAIDI

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi

Baadhi ya Wananchi wa Chindi na Ntinga wakiwa katika Harakati za Kuvuka Mto

Walazimika kulipa hadi 8000 kuvuka mto kwa mtumbwi

Mohamedi Mchengerwa, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Wanaozuia watumishi kupanda vyeo wakaliwa kooni

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ

Muonekano wa Eneo la Somanga baada ya Mawasiliano kati ya Lindi na Dar es Salaam kurejeshwa.

Mawasiliano yarejeshwa barabara ya Dar - Lindi

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga

Kituo cha kupoza umeme kujengwa Tunduma

Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Charles Bukombe, akizungumza na abiria

"Fungeni mikanda muda wapo safarini" - SSP