Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Alph Lukau 'aliyefufua' mtu, mapya yaibuka

Friday , 15th Mar , 2019

Kipindi cha habari za uchunguzi kinachorushwa na kituo cha Shirika la Utangazaji Afrika Kusini (SABC) kinachoitwa Cutting Edge, kimebaini mapya kuhusu mchungaji Alph Lukau.

Kipindi hicho ambacho kimerushwa siku ya Jumanne ya wiki hii, kimebaini kuwa mchungaji huyo mwenye asili ya Kongo amekuwa akiwafuata watu msikini na kuwalipa, ili waende kutoa ushuhuda wa uongo kwenye kanisa lake, kwa ajili ya kuvutia watu wengi zaidi.

Uchunguzi wa kina wafanyika 

Uchunguzi umebaini kuwa watu wengi waliongea tofauti na kile walichotarajia, kwa kuumbua matendo mabaya ya mchungaji huyo aliyedai kumfufua mtu hivi karibuni.

Samantha Revesai ambaye aliaminiwa kuwahi kuponywa UKIMWI na mchungaji huyo, amefunguka na kusema kwamba mchungaji Lukau alimfuata na kupanga naye dili, na kisha kwenda kanisani  kujifanya ni muathirika wa UKIMWI ili amuombewe.

"Sikuwa muathirika na wala sijawahi kuwa muathirika, walitaka niigize kama mtu aliyeathirika na UKIMWI, kisha mchungaji akaniombea na kuniponya, ili wavutie watu wengi waje kanisani”, amesema Samantha.

Lakini licha ya habari hizo zote mwanasheria wa kanisa hilo bado hajazungumza lolote, na msemaji wa kanisa hilo Bui Gaca amekanusha taarifa hizo na kusema kwamba ni uongo unapangwa kumchafua Mchungaji Lukau.

Mchungaji Lukau alipata umaarufu zaidi mwishoni mwa mwezi uliopita baada ya kutrend kwa habari ya kumfufua mtu, ambaye baadaye ilikuja kujulikana na mwenyewe kukiri kuwa mtu huyo hakuwa amefariki dunia.

mchungaji aliyefufua mtu akiwa katikati ya maombi ya kumfufua mtu huyo

HABARI ZAIDI

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala