
Azam FC ina nafasi kubwa ya kukutana na Bidvest, ambayo imetoka kushinda mabao 3-0 dhidi ya Light Stars ya Shelisheli kwenye mchezo wa raundi ya awali ya michuano hiyo na sasa watacheza mchezo wa marudiano, jijini Johannesburg, Afrika Kusini wikiendi hii.
Mchezo wa kwanza baina ya Azam FC na Bidvest Wits unatarajia kufanyika Machi 12 mwaka huu kwenye uwanja wa Bidvest jijini Johannesburg saa 12.00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki kabla ya kurudiana nao Azam Complex Machi 20 mwaka huu saa 9.00 Alasiri.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amesema kuwa kambi hiyo maalumu wataiweka kwenye nchi jirani na Afrika Kusini kwa siku nne kabla ya kuelekea jijini Johannesburg siku moja kabla ya mchezo huo.
“Tunamshukuru mwenyezi Mungu, tulipata nafasi ya kwenda jijini Ndola (Zambia), ile ilikuwa ni sehemu yetu ya kujiandaa na mechi za Kimataifa, watu walitubeza lakini tunasema ndio hivyo na kwa maana ya kuelekea kwenye mechi hiyo kocha kashaweka programu yake na tayari utawala umeshaifanyia kazi programu hiyo".Alisema Kawemba.