Tuesday , 22nd Jan , 2019

Kama kuna mamlaka ya mapato ambayo inashughulika na majina makubwa kwenye suala la kodi, basi ni 'Spanish Tax Agency' (STA), ambayo imeshawafikisha mahakamani na kuwakuta na hatia nyota mbalimbali wa soka Duniani na nchini humo.

Jose Mourinho na Cristiano Ronaldo walipokuwa mahakamani kwa nyakati tofauti.

Leo Januari 22, 2019 Mahakama ya mjini Madrid nchini Hispania imemkuta na hatia ya kukwepa kodi nyota wa zamani wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, ambaye sasa amepigwa faini ya £16.5 millioni, zaidi ya shilingi bilioni 43.

Ronaldo mwenye miaka 33 amekubali kulipa fainali hiyo ili kuepuka kwenda jela kwa miezi 23 kutokana na sheria za Hispania kuruhusu mtu ambaye amekutwa na hatia kwa mara ya kwanza kulipa faini badala ya kwenda jela.

Mbali na Ronaldo watu wengine ambao wamewahi kukutwa na hatia ya kukwepa kodi nchini Hispania ni Lionel Messi pamoja na Jose Mourinho.

Mwezi Septemba 2018, kocha Jose Mourinho alikutwa na hatia ya kukwepa kodi ambapo alipigwa faini ya £1.78m zaidi ya bilioni 2. Julai 2017 Lionel Messi alikutwa na hatia ya kukwepa kodi na kupigwa faini ya €5m zaidi ya shilingi bilioni 5.

Nyota wengine ambao wamewahi kukutwa na hatia ya kukwepa kodi nchini Hispania ni
Javier Mascherano, Angel di Maria, Cristiano Ronaldo, Samuel Eto'o, Radamel Falcao na wakala wa Ronaldo Jorge Mendes.