Wednesday , 10th Dec , 2014

Shirikisho la Ngumi nchini BFT, limesema linatarajia kuanza kuzungukla mikoani ili kuweza kupata vipaji vipya vya ngumi nchini vitakavyoweza kushiriki mashindano makubwa ya ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na East Africa Radio, Mjumbe wa maendeleo ya wanawake Tanzania kutoka BFT, Aisha Voniatis amesema mpaka sasa wamepata vipaji mbalimbali vya wanawake katika mashindano ya ngumi taifa ambao wanatarajia kuunda timu ya taifa ya muda mrefu ya wanawake.

Aisha amesema watakapopata vijana kutoka mikoani watawaunganisha vijana hao na timu ya taifa ili kuweza kufanya maandalizi ya mashindano ya Ngumi ya Dunia yanayotarajiwa kufanyika mwakani nchini Brazil.

Aisha amesema,katika upande wa ngumi za wanawake, makocha wamejitokeza kwa wingi kutoka vilabu mbalimbali nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa mabondia wanawake.