Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Bocco asimulia alivyotendwa mitandaoni

Monday , 22nd May , 2017

Nahodha wa Azam FC, John Bocco, hivi karibuni amejikuta akiingia matatizoni na uongozi wa klabu yake baada ya wajanja wa mtandaoni kumzidi ujanja.

Nahodha wa Azam, John Bocco

Taarifa kutoka klabuni hapo zimedai kuwa ukurasa wa Instagram wa Bocco, Ijumaa iliyopita ulivamiwa na matapeli wa mtandaoni na kuanza kuandika mambo mbalimbali kuhusiana na mchezaji huyo, jambo ambalo liliushitua uongozi wa klabu hiyo.

Moja kati ya mambo hayo yaliyoandikwa katika ukurasa huo ni: “Kuna wakati wa kuondoka hata kama hujui pa kwenda, ondoka wajue thamani yako.”

Maneno hayo yaliwachanganya vilivyo viongozi wa timu hiyo, baada ya kuyaona katika ukurasa huo, jambo ambalo lilisababisha wamuulize alikuwa akimaanisha nini.

Bocco amesema kuwa, hali hiyo ilimsababishia usumbufu mkubwa kwani watu wengi waliamini kuwa yeye ndiye aliyeandika maneno hayo licha ya kuwaambia ukweli kuhusiana na kilichotokea.

“Nawaomba watu wote waelewe kuwa sina tatizo na Azam na wala siyo mimi niliyeandika maneno hayo, bali ni matapeli ambao wamevamia ukurasa wangu wa Instagram tangu juzi (Ijumaa) na wamekuwa wakiandika mambo yao hayo huku nikiona.

“Hata hivyo nimeshatoa taarifa sehemu zinazohusika lakini pia nimeamua kufungua ukurasa mwingine wa Instagram,” alisema Bocco ambaye anadaiwa mkataba wake na Azam umemalizika, hivyo inadaiwa kuwa ametumia mbinu hiyo ili kushtua uongozi wake uweze kumpatia mkataba mwingine.

Alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema: “Huo ni uzushi tu ambao hauna ukweli wowote, mimi bado nina mkataba na Azam na kama utamalizika na wakiwa bado wananihitaji wataniambia, hivyo siwezi kufanya hivyo hata siku moja.”

Viongozi wa Azam FC hawakuweza kupatikana jana kuzungumzia suala hilo, kutokana na simu zao za mkononi kuita tu bila ya kupokelewa.

HABARI ZAIDI

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi

Baadhi ya Wananchi wa Chindi na Ntinga wakiwa katika Harakati za Kuvuka Mto

Walazimika kulipa hadi 8000 kuvuka mto kwa mtumbwi