Sunday , 16th Mar , 2014

Siku chache kabla ya pambano bondia afariki akijiandaa

Tasnia ya mchezo wa masumbwi nchini hii leo imepata pigo kubwa kufuatia kifo cha bondia mahili wa ngumi za kulipwa nchini Fadhili Ahwadh aliyefariki hii leo baada ya kuugua ghafla kufuatia kupata maumivu wakati wa mazoezi ya juzi akijiandaa na mpambano wake dhidi ya Kamote toka Tanga

Na kuhusiana na taarifa hiyo ya kifo cha bondia Fadhili Ahwadh tunaye bondia bingwa wa dunia mtanzania Francis Cheka aliyekua na marehemu siku moja kabla ya bondia huyo kufikwa na umauti akituthibitishia hilo

Cheka amesema kuwa marehemu juzi alikua kwenye mazoezi ya kawaida akijiandaa na mchezo wake wa ubingwa wa UBO dhidi ya bondia Kamote toka Tanga mpambano ambao ungefanyika march 29 mwaka huu na ndipo alipopata tatizo wakati akiendelea na mazoezi yake

Baada ya hapo alikimbizwa hospitali ya Sinza na hali ilipozidi kuwa mbaya akahamishiwa hospitali ya Mwananyamala ambako ndiko alifikwa na umauti,marehemu enzi za uhai wake alicheza mapambano mengi na alifanya vema.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema, Amen.