Wednesday , 18th May , 2016

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa hakuchaguliwa katika kikosi cha Uhispania cha Euro 2016.

Kocha Vicente Del Bosque pia amemuacha nje kiungo wa kati wa Manchester United Juan Mata pamoja na aliyekuwa mshambuliaji wa Liverpool na Chelsea Fernando Torres.

Mabingwa watetezi Hispania wako katika kundi D pamoja na Croatia, Czech na Uturuki wakiwania taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo.

Diego Costa amefunga bao moja tu katika mechi 10 akiichezea Hispania.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alikosa kucheza mechi mbili za mwisho za klabu yake Chelsea kutokana na jeraha la mguu.

Wachezaji wengine walioachwa nje ya kikosi ni beki wa Bayern Munich Javi Martinez na kiungo wa kati wa Arsenal Santi Carzola huku kocha Del Bsoque akimshirikisha Saul Niguez wa Atletico Madrid na Lucas Vazquez wa Real Madrid.