
Dismas Ten na Mashabiki wa Simba
Dismas Ten ambaye ni msemaji wa zamani wa Mbeya City, amewaambia Simba kuwa watakaa nafasi hiyo mpaka mwisho wa ligi mwezi Mei 2019.
''Umejiunga na kifurshi cha kukaa nafasi ya tatu, tumia mpaka Mei 30, 2019 salio lako ni Tsh. Bilioni 1.3 asante kwa kushiriki'', ameandika Dismas kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Yanga jana ilishika usukani wa ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kushinda mchezo wake wa 13 dhidi ya JKT Tanzania kwa mabao 2-0 hivyo kufikisha alama 35 na kuizidi Azam FC yenye alama 33, jambo ambalo linampa matumaini Dismas Ten kwa klabu yake kuendelea kukaa katika nafasi hiyo hadi mwisho wa msimu.
Simba kwasasa ipo nafasi ya 3 ikiwa na alama 27 kwenye mechi 12 ilizocheza.