Tuesday , 6th Jun , 2017

Gor Mahia wamefuzu kuingia nusu fainali ya Sportpesa Super Cup baada ya kuwachapa Jang'ombe ya Zanzibar bao 2-0 mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Mabao hayo yamepatikana kupitia mshambuliaji wake Meddie Kagere kipindi cha pili cha mchezo dakika 63 na 83 baada ya mtifuano mkali kutoka kwa Jang'ombe walionekana kukata tamaa baada ya kupachikwa bao la pili.

Kutokana na ushindi huo, Gor Mahia imekuwa timu pili kutoka Kenya na ya tatu  kuingia moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Sportpesa Super Cup baada ya Mabingwa watetezi ligi kuu Tanzania Bara Yanga pamoja na AFC Leopard ya Kenya kufuzu kwa siku ya jana Jumatatu.

Kikosi cha Jang'ombe kilikuwa; Ruga H.Haroun, ALmas s Said, Maundu M Issa, Said I Mohamed, Amour F Seif, Chandika I NOvat, Ali Abdul S Kassim, Abdi A Kassim, Abdalla R Mohamed, Makame K Mussa, Juma H Barik wachezaji waakiba wakiwa ni Ali sa, Abdallah HS, Abdallah HC, Makame Suleiman, Bakari Y A, Mwinyi IS.

Gor Mahia,Haron Shakava, Fredrick Odhiambo, Wellington Ochieng, Joash Onyago, Philemon Odhiambo, Francis Kahata, Kenneth Muguna, Timothy Otieno, Medie Kagere, Mike Simiyu wachezaji wa akiba wakiwa ni Shaban Odhoji, Bernard Odhiambo, George Odhiambo, Antony Mbugua, Amos Nonsi, Teddy Osok.